Change is here! We are now Fin Tanzania (formerly Fikia Finance).

Uthibitisho Wa Mkopaji

1. UTHIBITISHO WA MKOPAJI
Mimi mkopaji, nathibitisha na kukubali kuwa:
a)  Nimeona mtiririko wa taaarifa katika fomu hii inayoonesha taarifa kamili kuhusu malipo yote ninayotakiwa
 kufanya endapo nitapatiwa mkopo (”Mkopo”) na zinafanana na zile nilizooneshwa kabla ya kusaini makubaliano
 (Makubaliano);

b)  Nimeelewa vigezo vya Makubaliano kama nilivyoelezewa kwa lugha ninayoielewa (Kiswahili), pamoja na masharti
 ya Mkopo uliopendekezwa;

c)  Nimesoma au nimesomewa Makubaliano;

d)  Endapo makato yatafanyika katika mshahara wangu kutokana na Makubaliano haya, makato hayo yataendelea bila 
    kusitishwa mpaka pale nitakapomaliza kulipa Mkopo wote kikamilifu.

e)  Nimepatiwa nakala ya Makubaliano haya, pia

f)  Nimeelezewa taratibu za kutoa malalamiko.

g)  Ikiwa nitaondoa maombi baada ya mchakato kuanza, nitawajibika kwa kurudisha gharama alizoingia Mkopeshaji.

2. KIBALI KUTOKA KWA MKOPAJI
Mimi Mkopaji, nampa Mkopeshaji (Fikia Finance Limited) mamlaka na idhini ya:
a)  Kuwasiliana na mtu yeyote kuhakiki kuwa taarifa nilizowasilisha kwenye maombi haya au katika Makubaliano,
    bima au mahali pengine ziko sahihi;

b)  Kupata taarifa kutoka mahali popote kuhusu hali yangu ya kifedha na taarifa za benki, pamoja na historia 
    ya mikopo na malipo;

c)  Kutoa taarifa za mkopo huu mahali popote , ikiwemo taasisi ya taarifa za mikopo;

d)  Kuhamisha mamlaka na shughuli zake tajwa katika makubaliano haya kwenda kwa mtu au ofisi yoyote;

e)  Kutoa taarifa kwa jeshi la polisi la Tanzania au mamlaka yoyote husika endapo itagundulika kuwa nimefanya
 udanganyifu au kwa makusudi nimeficha taarifa muhimu katika maombi/Makubaliano haya

f)  Kutumia taarifa zitokazo katika taasisi ya utunzaji na uchakataji wa taarifa za mikopo
 (CREDIT REFERENCE BUREAU) chini ya kanuni za Benki Kuu ya Tanzania, au taratibu halali za mamlaka 
hii katika mchakato wa kunipatia mkopo na pia kurudisha taarifa hizo katika taasisi ya utunzaji na 
uchakataji wa taarifa za mikopo kwa ajili ya utunzaji wa taarifa hizo.

g)  Kwamba taarifa hizi zitaendelea kutumika na mamlaka husika hata baada ya muda wa Mkopo kwa 
kuzingatia sheria na kanuni za utoaji wa taarifa husika.

3. UHALALI WA MKATABA
a)  Makubaliano haya hayatavunjwa kwa namna yoyote ile ndani ya kipindi cha Mkopo kati ya mimi Mkopaji
 na mkopeshaji isipokuwa tu pale Mkopo utakapomalizika kikamilifu

b)  Makubaliano haya ni moja ya makubaliano kati ya Mkopaji na Mkopeshaji na mabadiliko yoyote 
yatatakiwa kuwa katika maandishi na kutiwa saini na Mkopaji pamoja na Mkopeshaji.

4. ULIPAJI WA MKOPO
a)  Baada ya Mkopaji kupatiwa kiasi chote cha Mkopo, Mkopaji atadaiwa na Mkopeshaji kiasi chote 
cha Mkopo kilichopo kwenye Makubaliano haya kulingana na Mkataba wa kukopa.

b)  Mkopo wote utatakiwa kurejeshwa katika mafungu yanayolingana kama ilivyokubaliwa katika 
Mkataba wa kukopa.

c)  Mkopeshaji atapokea marejesho na malipo yote ya Mkopo kupitia kwenye akaunti ya benki ya Mkopeshajii.

d)  Mkopaji hataruhusiwa kufanya malipo ya pesa taslimu kwa muajiriwa, wakala au afisa yeyote wa Mkopeshaji.

e)  Malipo yote ya Mkopo yatafanyika katika mpangilio ufatao;
  i.Gharama za kisheria;
  ii.Gharama za nyongeza/ riba ya kushindwa kulipa;
  iii.Gharama kamili za Mkopo; Pamoja na;
  iv.Salio la Mkopo aliopatiwa mkopaji.

5. MALIPO YA MAPEMA
a)  Mkopaji ana haki ya kulipa kiasi chote cha Mkopo ndani ya siku tatu za kazi bila kuingia 
gharama yoyote, ili mradi malipo hayo yanafanywa kwenye akaunti ya benki ya Mkopeshaji.

b)  Kufuatia fomu hii, ada ya mchakato haitarejeshwa kwa Mkopaji endapo atakamilisha malipo
 yake mapema.

   i. Mkopaji anaweza kulipa kiasi cha Mkopo ambao bado anadaiwa katika makubaliano haya tarehe 
yoyote aliyopangiwa kufanya malipo, au mara moja katika mwezi wowote bila faini yoyote.
  ii. Mkopaji anaweza kumaliza malipo yaliyokubaliwa mapema zaidi kwa kulipa kiasi chote 
anachotakiwa kulipa.
  iii. Kiasi kinachotakiwa kulipwa ni jumla ya malipo yafuatayo:
    a.   Salio la Mkopo ambalo bado halijalipwa mpaka tarehe ya mwisho wa Makubaliano; pia
    b.   Kiasi cha riba na tozo/ malipo mengine yote ambayo Mkopaji anatakiwa kumlipa Mkopeshaji
 mpaka hapo anapokamilisha malipo ya mapema.

iv.  Kufahamu kiasi sahihi cha kulipa, Mkopaji ana haki ya kupata taarifa ya malipo hayo 
kutoka kwa Mkopeshaji.

6.  KUSHINDWA KULIPA DENI NA HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA.
a) Mkopeshaji atakuwa na haki ya kudai mara moja malipo yote ya deni lililobakia endapo mkopaji:
i.  Atakwenda kinyume na Makubaliano haya;
ii.  Atafilisika; 
iii. Atakufa; 
iv.  Atapata ulemavu wa kudumu kiasi cha kushindwa kulipa ; 
iv.  Alitoa utambulisho wa uongo alipokuwa akiomba Mkopo; 
v.   Atafanya kitu chochote kinachoweza kuhatarisha haki ya Mkopeshaji kulingana na mkataba huu; au 
vi.  Atapoteza ajira yake mahali ambapo makato yake ya Mkopo yalikuwa yakipunguzwa kutoka kwenye mshahara wake. 

b) Mkopeshaji hatapoteza haki zake nyingine za kisheria Kwa kutumia haki yake ya kudai malipo ya Mkopo
 kwa mara moja.

c) Mkopaji anakubali kwamba, endapo Mkopeshaji ameingia gharama za kutimiza Makubaliano haya, Mkopaji 
atawajibika kufidia gharama hizo.

7.  MAOMBI NA KUIDHINISHA/ KUKATALIWA
a) Mkopaji hatapata haki ya moja kwa moja kupata Mkopo kwa kujaza na kusaini Makubaliano haya/
 Mkataba tu.

b) Mkopeshaji atakapoidhinisha na kukukbali kutoa Mkopo, Fomu hii itakuwa Makubaliano yatakayobana
 pande zote mbili kati ya Mkopeshaji na Mkopaji.

c) Mkopeshaji atabaki kuwa na haki ya kubadilisha vigezo na masharti ya Mkopo itakavyofaa.

d) Iwapo maombi ya Mkopo yatakataliwa, Mkopeshaji hatalazimishwa kutoa sababu.


8. UTOAJI WA MKOPO NA KURIDHIA
a) Mkopo utalipwa/utatumwa kwenye akaunti ya benki iliyotajwa na Mkopaji kwenye fomu hii.

b) Mkopaji anakubali kuwa Mkopeshaji hatawajibika kwa  uharibifu/upotevu wowote utakaosababishwa 
na malipo yatakayofanywa katika akaunti iliyoletwa na Mkopaji.

c) Kama malipo hayajafanyika ndani ya siku tatu za kazi, Mkopaji atawasiliana na Mkopeshaji na
 kuonesha ushahidi wa kutopokea malipo hayo.

9. RIBA NA GHARAMA ZINGINE ZA MKOPO
a)  Riba itakayolipwa kwenye Mkopo itakuwa ya kiwango cha kudumu, itahesabiwa na kuongezwa juu 
ya malipo ya kipindi chote kulingana na ratiba ya marejesho.

b)   Kiasi cha Riba ni asilimia 3.5 kwa mwezi kwa njia ya kupungua sawasawa na maelezo ya kifungu 9(a)
 cha RIBA.  

c)  Iwapo Mkopaji atashindwa kufanya malipo ndani ya tarehe iliyobaliwa au endapo Mkopeshaji atasogeza
 muda wa malipo, riba ya Mkopo unaodaiwa itajumuishwa na kuwa sehemu ya Mkopo kwa mwezi unaofuata.
 Riba iliyokubaliwa hapo awali itatozwa juu ya jumla mpya ya Mkopo.

d) Itakapomlazimu Mkopeshaji kuchukua hatua ili kudai na kupata malipo ya Mkopo, malipo yatatakiwa 
kuongezewa riba ya kiwango cha kudumu kama ilivyo katika fomu hii

e)  Iwapo Mkopo utachelewa kulipwa, Mkopaji atatozwa 1% ya rejersho kwa kila siku atakayochelewa bila 
kuathiri makato ya kawaida yaliyokubaliwa katika Makubaliano haya. Tozo hiyo itatozwa baada ya Mkopaji
 kushindwa kulipa kulingana  tarehe ya malipo.

f)  Kiasi cha tozo ya mchakato ni asilimia 6 ya jumuisho la mkopo ulio ombwa na gharama zingine.

g)  Mkopaji anakubali kulipa gharama nyingine zitakazo ambatana na Mkopo huu.


10. BIMA YA MAISHA YA MKOPO 
a)  Mkopeshaji anamtaka Mkopaji awe na bima ya maisha ya Mkopo kwa ajili ya kipindi kizima cha Mkopo.
Mkopaji atapatiwa nafasi ya kuchagua kati ya bima iliyoamabatanishwa kwenye Mkopo au kutoa pendekezo 
la bima inayokidhi vigezo.

b) Endapo Mkopaji atachagua bima tofauti na ile ya Mkopeshaji, bima hiyo itatakiwa kuidhinishwa na 
Mkopeshaji na kuwekwa chini ya mamlaka ya Mkopeshaji.

c)  Endapo mkopaji atachagua bima ya maisha ya Mkopo iliyopendekezwa na Mkopeshaji bima ya maisha 
ya Mkopo itatolewa na Sanlam Life Insurance (T) Limited (“Sanlam”);

d) Mkopaji atalindwa na bima hii kwa kiasi cha mkopo katika Makubaliano haya endapo atafariki 
au kupata ulemavu wa kudumu;

e) Bima hii pia itamnufaisha Mkopeshaji endapo Mkopaji atafariki dunia, kama tu Sanlam atapokea 
uthibitisho wa kuridhisha juu ya kifo cha Mkopaji; pia

f) Taarifa zaidi juu ya bima hii zinapatikana kwenye fomu ya mpangilio wa bima ya maisha ya Mkopo.


11. UDADISI WA UWEZO WA KULIPA MKOPO
Kwa kutumia taarifa zitakazotolewa wakati wa kufanya uamuzi wa kutoa Mkopo pamoja na historia
ya ulipaji madeni ya mkopaji, Mkopeshaji atatakiwa kuzingatia mambo mbalimbali na kuamua kama
Mkopaji anakidhi vigezo vyote vya makubaliano ya Mkopo.


12. NYARAKA 
Cheti /Nyaraka iliyotiwa sahihi na Mkurugenzi wa Mkopeshaji inaweza kutumika kama kielelezo
cha kuonesha kiasi cha deni la Mkopo husika.


13. TAARIFA ZA MKOPO 
Taarifa za hali ya Mkopo zitatotelea kwa Mkopaji pindi zitakapohitajika na bila gharama za ziada.


14. SHERIA 
Makubaliano haya yamezingati sheria na kanuni za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


15. UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MKOPAJI 
Mkopeshaji,wafanyakazi wake na maafisa husika hawatatoa taarifa za Mkopo na miamala husika 
kwa mtu yeyote au taasisi yoyote isipokuwa:
i. Mkopaji ametoa ruhusa kwenye Makubaliano  haya;
ii. Mkopaji amethibitishwa kuwa amefilisika;
iii. Taarifa hizi zitahitajika katika mahitaji/matumizi ya sheria ama kesi mahakamani
iv. Taarifa itahitajiwa na Mkopeshaji mwingine ili kuangila hali ya mkopo uliopo endapo
Mkopaji ataamua kuchukua Mkopo katika kampuni nyingine ya ukopeshaji;
v.  Taarifa hii itahitajika na mamlaka nyingine kisheria; pia,
vi. Kama ni muhimu au lazima kisheria kutangaza kwa faida ya umma


16. MALALAMIKO
a) Endapo kutakuwa na malalamiko, Mkopaji atatakiwa kubainisha malalamiko yake husika kupitia
barua pepe hii tzinfo@fin.africa

b) Mkopeshaji atashughulikia malalamiko hayo kwa haraka,

c)  Malalamiko yasipofanyiwa kazi, Mkopeshaji atalalamika kwa njia ya maandishi.


17. ANUANI YA MKOPAJI
a)   Taarifa zote za Mkopaji zitatumwa katika anuani husika kama ilivyo ainishwa katika kipengele”A”.

b)  Taarifa yoyote itakayotumwa kwa Mkopaji kupitia barua pepe yake itachukuliwa kuwa imemfikia hapo
hapo iwapo itatumwa na Mkopeshaji akapata taarifa kuwa taarifa imetumwa kwenye anuani husika.

c) Mkopaji atatakiwa kutoa taarifa kwa maandishi endapo kama atabadili anuani yake.


18. UTHIBITISHO NA KUKUBALI
Mimi niliyesaini hapa chini: 
a)  Ninathibitisha kuwa taarifa zilizotolewa ni sahihi na za kweli na nina ahidi kutoa 
taarifa kwa Mkopeshaji kwa mabadiliko yatakapojitokeza siku za baadae yanayoweza kuathiri 
hadhi yangu kama mteja kwa Mkopeshaji.

b) Nitalipa fidia kwa Mkopeshaji kwa hasara au uharibifu utakaosababishwa na mimi kwa kutoa
taarifa zisizo sahihi, udanganyifu au zenye mapungufu.

c) Ninakubaliana na kanuni na masharti ya Mkopo na ninaahidi kuzifuata pamoja na taratibu
na miongozo iliyowekwa na itakayobadilishwa kwa kadiri ya mahitaji.

d) Nina uwezo wa kulipa Mkopo nilioomba.

e) Ninamruhusu Mkopeshaji kuhakiki taarifa zangu na kuuliza chanzo chochote pale inapolazimu
na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wangu wa kanuni na masharti ya Mkopeshaji wa kampuni
au ofisi nyingine ya mikopo kwa mujibu wa sheria, kanuni za maadili na taratibu zilizopo.

f) Nimeelewa ya kwamba nikitoa taarifa zisizo sahihi Mkopeshaji ana haki ya kukataa maombi yangu.

g) Nimesoma na kuelewa haki na majukumu yangu kama ilivyoelezwa kwenye vigezo na masharti.

h) Ninakubali kuendelea na mpangilio wa bima ya Maisha ya mkopo (credit life insurance) kwa utaratibu
uliopangwa na Mkopeshaji.

i) Tafadhali fahamu kwamba zoezi zima la kuchukua Mkopo litasimamishwa mpaka pale uamuzi wa kubadili
bima utakapokuwa umehitimitishwa.

j) Ikiwa Mkopaji atasitisha maombi ya Mkopo, atalazimika kulipia gharama ambazo Mkopeshaji itakuwa
imeingia hadi wakati huo wa kusitisha.